Majibu ya Guardiola kuhusu kipigo dhidi ya Spurs yashangaza ‘Ni matokeo bora zaidi kuliko sare ya 0 – 0’


Majibu ya kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola kuhusu kipigo walichopata kutoka kwa Tottenham cha 1 – 0 mchezo wa robo fainali Champions League yashangaza.
Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola

Pep Guardiola amesema kuwa Manchester City kupoteza kwa bao 1 – 0 dhidi ya Tottenham ni matokeo bora zaidi kuliko ingekuwa sare tasa ya 0 – 0 kwenye michuano hiyo hiyo ya Champions League hatua ya robo fainali.

Heung-Min Son ndiyo alikuwa mwiba mkali kwenye mechi hiyo kwa kuisaidia timu yake ya Spurs kupata ushindi huo baada ya kupachika bao pekee lililodumu hadi dakika 90 za mchezo.
Heung-Min Son

Guardiola amesema “Inatufanya hali hii kuwa kwenye nafasi ya pili, lakini wakati mwingine matokeo ya 1 – 0 ni bora zaidi kuliko 0 – 0 kwasababu unafahamu hasa nini chakufanya.”

“Ikiwa ni 0 – 0, inakufanya ufikirie mchezo wa marudiano ujilinde au ushambulie lakini kwa sasa tunafahamu ni lazima kufunga mabao.”

”tTutafanya uchambuzi wa mechi, lakini kwa wakati huu nafikiri tumecheza vizuri, tuliutawala mchezo.”

Hata hivyo vijana wa, Guardiola walipuga shuti moja peke lililolenga lango kutokea dakika 13 na kupata penati iliyokolewa na mlindalango, Hugo Lloris.
1

Post a Comment

0 Comments