Lucas Moura alifunga hat trick wakati timu yake Tottenham ikiipiga Huddersfield ambayo tayari imeshushwa ngazi mabao 4 – 0. Moura sasa ni Mbrazil wa nne kufunga hat trick katika Premier League. Mkenya Victor Wanyama alifunga bao jingine la Spurs ambao wamepanda hadi nafasi ya tatu mbele ya Chelsea ambao wana mechi dhidi ya Liverpool Jumapili.
Paul Pogba alifunga mabao mawili kupitia penalty wakati Manchester United iliifunga West Ham 2 – 1 na kusonga juu ya Arsenal katika nafasi ya tano pointi mbili nyuma ya Chelsea ambao wana pointi 66.
from sokoa news http://bit.ly/2GhQjYO
1

0 Comments