Yanga yaendeleza kipigo kwa kulamba sukari ya Kagera

Mabingwa wa kihistoria kwenye ligi kuu Tanzania bara (27) Yanga imeibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa TPL uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.

Yanga ikiwa imetoka kupata ushindi dhidi ya African Lyon wa goli 2-0 hapo hapo Kirumba ilitanguliwa kufungwa kwa mpira wa kona uliomaliziwa kwa umaridadi mkubwa na nahodha wa Kagera Paul Galikyoma Gwai dakika ya 30 kabla ya Khasim Hamisi kujifunga dakika 5 baadae kwa mpira uliopigwa na Papy Kabamba Tshishimbi.

Mpaka dakika ya 45 zinamalizika mambo yalikuwa 1-1.

Kipindi cha pili kikawa na magoli bora kabisa, mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Heritier Makambo akatia kimiani goli kwa kichwa akimaliza mgongeo wa mbali kutoka kwa Kelvin Yondani.

Dakika chache baadae Hassan Khamisi akasawazisha goli kwa shuti kali lililompita kipa Klaus Kindoki ambaye pia ni Mcongomani baada ya kuzembea kwa Paul Godfrey.

Wakati dakika zikiyoyoma kuelekea kipenga cha mwisho Nahodha wa Yanga kwa mchezo huo Thaban Sinkara Kamusoko aliumalizia mpira uliotengwa kwa msaada wa Gadiel Michael baada ya makosa ya mlinda mlango wa Kagera Sugar.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 74 nafasi ya kwanza.

Hii inakuwa mara ya pili kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Kagera Sugar kuzalisha kadi nyekundu baada ya Yondani kwa kadi nyekundu, msimu uliopita wakati Mbaraka Yusuf yupo Kagera alionyeshwa kadi nyekundu.

Mbali na tukio hilo, mlinzi Kelvin Yondani wa Yanga ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya mchezo usio wa kiungwana kwa Paul Mwalyazi, jambo lililopelekea Yanga kuwa pungufu mpaka kipenga cha mwisho kinapigwa.

Mchezo mwingine uliopigwa April 10, 2019

Singida United 0-0 KMC




from sokoa news http://bit.ly/2v0xUuE
1

Post a Comment

0 Comments