LACAZETTE APIGA MBILI ARSENAL IKIIUA 3-1 VALENCIA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE

Mshambuliaji Mfaransa, Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifungia Arsenal mabao mawili dakika za 18 na 25 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Valencia kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Emirates mjini London. Bao la tatu la Arsenal lilifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 90, wakati la Valencia lilifungwa na Mouctar Diakhaby dakika ya 11 na timu hizo zitarudiana Mei 9 Uwanja wa Mestalla mjini Valencia na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Chelsea na Eintracht Frankfurt kwenye fainali Mei 29 PICHA ZAIDI SOMA HAPA 




from sokoa news http://bit.ly/2UWCcNW
1

Post a Comment

0 Comments