Mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kupigwa saa tisa Alasiri



Mabingwa wa Tanzania Bara Simba watakamilisha msimu mkoani Morogoro kwa kuumana na Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa Jamhuri

Baada ya mchezo huo, Simba mabingwa hao wa nchi watakabidhiwa taji la ligi kuu walilolitwaa kwa msimu wa pili mfululizo

Uongozi wa Mtibwa Sugar ambao ndio wenyeji wa mchezo huo, wamethibitisha kuwa utaanza saa tisa Alasiri

"Mchezo wetu wa mwisho wa ligi kuu bara (TPL) dhidi ya Simba utachezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro Mjini, Jumanne, 28.05.2019"

"Mchezo huo utaanza saa 9:00 mchana na awali ulipangwa kuchezwa saa 10:00. Sababu ya kubadili muda ni kupata muda wa kutosha wa sherehe za kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi kuu bara kwa mujibu wa bodi ya ligi," imesema taarifa ya Mtibwa Sugar

Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es salaam mapema leo tayari kwa mchezo huo na shamrashamra za ubingwa


from sokoa news http://bit.ly/2JJQGzE
1

Post a Comment

0 Comments