Na Amiri kilagalila-Njombe
Kituo kimoja na familia nne zinazoishi katika mazingira hatarishi kata ya Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo, zimekabidhiwa msaada wa kijamii ikiwemo mafuta ya kupikia kutokana na uhitaji wa familia hizo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mahitaji hayo, Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata mwenda, amesema kuwa halmashauri yake kila mwaka katika bajeti ya kitengo cha ustawi wa jamii kupitia mapato ya ndani imekuwa ikiweka bajeti kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji.
“Sisi kila mwaka katika bajeti yetu kitengo cha ustawi wa jamii huwa tunaweka bajeti kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji,na safari hii tumeanza kutoa misaada kupitia mapato yetu ya ndani shilingi milioni 5 na laki 4 na tutagawa kwa kaya 17 ambazo zina hali mbaya sana”
Veronicka Myango ni afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya mji wa Njombe, ametoa wito kwa jamii kuona umuhimu wa kutoa msaada wa haraka kwa familia zenye mahitaji ili kupunguza baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo.
Kwa upande wake Oliva Mtewele mwenye watoto watatu, mjane mkazi wa kijiji cha Makanjaula ambaye amefikiwa na msaada huo amesema kuwa amekuwa akijishughulisha na kilimo ili kuisaidia familia yake na kuishukuru serikali kwa kumtembelea na kumkabidhi msaada ikiwemo godoro.
from sokoa news https://ift.tt/2XpxGc0
1
0 Comments