Johari Hajawahi Kumnyima Chuchu Usingizi

Blandina Chagula ‘Johari’.

ZANZIBAR Mwanamama kunako Bongo Muvi, Chuchu Hans, kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa, hajawahi kutikiswa na mwigizaji mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kiasi cha kukosa usingizi, kisa penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda kwenye kambi maalum iliyoandaliwa na Swahiliflix visiwani Zanzibar, Chuchu alisema siku zote mwanamke anatakiwa kujiamini kuwa hakuna neno la kusikia litakalomtikisa au kukunyima raha usingizi.

“Manenomaneno kuhusu Johari na Ray hayajawahi kuninyima usingizi kwa sababu ninajiamini na ninajua baba Jayden (Ray), nimepangiwa na Mungu,” alisema Chuchu

The post Johari Hajawahi Kumnyima Chuchu Usingizi appeared first on Global Publishers.




from sokoa news https://ift.tt/2yifTJB
1

Post a Comment

0 Comments