Kocha wa Yanga SC Mwinyi Zahera aibua jipya kuhusu Ibrahim Ajib


Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amefunguka na kusema hakushangaa Ibrahim Ajib kuondoka Yanga kwani hakuwa katika mipango yake kutokana na yeye alijua anaenda TP Mazembe.

Ibrahim Ajib Migomba kwa hivi sasa amerudi Simba SC na kusaini mkataba wa miaka miwili lakini alikuwa akihitajika na club ya TP Mazembe.

“Mimi wakati Ligi inamalizika Ajib sikumuweka kwenye mipango yangu nilikuwa najua kuwa hawezi kunisumbua, kwa sababu alikuwa kashasema ataenda TP Mazembe nilivyosikia anaenda nikasema hakuna shida kuna wachezaji wengine wazuri" amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Uamuzi wake (Simba) mimi sijui labda aliogopa TP Mazembe hatocheza kwa sababu mimi nilisumbuliwa na kocha wa TP Mazembe na President wao (Katumbi) alikuja hapa sasa wote wakashangaa kusikia Ajib anasema alipewa pesa ndogo”





from sokoa news https://ift.tt/2Xv1fZT
1

Post a Comment

0 Comments