Mashirika ya ndege ya British Airways la Uingereza na Lufthansa la Ujerumani yamesitisha ghafla safari za kwenda Cairo, nchini Misri kufuatia wasiwasi wa kiusalama, ingawa hayakueleza kwa kina kuhusu wasiwasi huo.
British Airways ndio iliyoanza kwa kusimamisha safari zake kwa siku saba, kuanzia jana Jumamosi, kama tahadhari ili kuruhusu kufanyika tathmini ya kina. Lufthansa pia ilisitisha safari zake za Misri kutokea Munich na Frankfurt, lakini lenyewe likisema lilikuwa linafuatilia hali ilivyo.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema ndege zinazotoka Misri kwenda Uingereza pia zilipitia hatua za nyongeza za kiusalama, huku ikiwataka abiria kutoa ushirikiano kamili na maafisa wa usalama kwenye viwanja vya ndege.
Maafisa wa Misri walinukuliwa kwa masharti ya kutotajwa majina yao wakisema mashirika mengine ya ndege yalikuwa yakiendelea na safari kama kawaida. Lufthansa nayo baadae ilisema inataraji kurejesha safari zake hii leo.
from sokoa news https://ift.tt/32JmbjM
1
0 Comments