Mauaji ya watoto Ufilipino yalalamikiwa


Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International imelalamika mauaji ya kiholela yanayotokea nchini Ufilipino yaliyofikia kiwango cha kutisha katika juhudi zinazofanywa na serikali za kupambana na mihadarati.

Uchunguzi uliofanywa na shirika hilo la haki za binadamu umeonyesha kwamba mauaji hayo yanakaribia uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Shirika hilo linataka uchunguzi huru ufanyike chini ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Serikali ya Ufilipino imesema matukio zaidi ya 6000 yametokea kuhusiana na mauaji hayo lakini shirika la Amnesty International linatuhumu kwamba idadi ya watu waliouliwa ni kubwa zaidi.


from sokoa news https://ift.tt/2JlD3oJ
1

Post a Comment

0 Comments