Msanii Taylor Swift aongoza kwa kulipwa fedha nyingi duniani


Akiwa chini ya umri wa miaka 30, Staa wa muziki kutoka Marekani, Taylor Swift ndiye Staa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kulingana na ripoti ya jarida maarufu la Forbes.

Ripoti hiyo iliwekwa hadharani Jumatano hii ambapo inasema anaingiza kibindoni $185m, akifuatiwa kwa karibu na Kylie Jenner anayeingiza kiasi cha $170m huku Rapper Kanye West akishika number 3, akitajwa kuingiza kiasi cha $150m.

Kupitia jarida la Forbes, mhariri wake na Taylor Swift, Zack O’Malley amesema sehemu kubwa ya mapato hayo yametokana na maonyesho ya jukwaani.




from sokoa news https://ift.tt/2XUoaSB
1

Post a Comment

0 Comments