Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema kuanzia msimu huu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho itakuwa mechi moja tu katika Uwanja maalum utakaoteuliwa.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa CAF, Amaju Pinnick katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari Jumatano na kwamba maelezo zaidi yatatolewa baadaye.
Lakini uamuzi huo umeonekana kupingwa vikali na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamba kulingana na miundombinu ya Afrika, hali ya kiuchumi no tofauti na Ulaya kuna hatari mechi hizo bila kuwa na watazamaji wengi uwanjani.
Mechi mbili za fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu hazikukamilika baada ya Wydad Casablanca ya Morocco kugombea mchezo wa marudiano na wenyeji, Esperance mjini Tunis nchini Tunisia dakika ya 59 wakipinga maamuzi ya refa kukataa bao lao ambalo lingekuwa la kusawazisha.
Kutokana na mechi kuvunjika, Esperance wakapewa Kombe na kutawazwa kuwa mabingwa wa Afrika , lakini uamuzi huo ulitenguliwa na Kamati ya Utendaji ya CAF iliyoagiza marudio ya mchezo huo, ingawa timu zilikata rufaa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimichezo (CAS) kila moja ikitaka ipewe ubingwa.
from sokoa news https://ift.tt/2XOLIJd
1
0 Comments