Viongozi wa Afrika watakutana leo nchini Niger kwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wa kutia saini makubaliano ya kihistroria ya biashara huru na kujadilia mzozo wa usalama na uhamiaji unaohofiwa barani humo.
Kulingana na mwenyekiti wa muungano huo Moussa Faki, kongamano hilo la kihistoria la kundi hilo la mataifa wanachama 55,viongozi wa mataifa hayo watazindua rasmi eneo huru la kibiashara la bara Afrika wakati wa kongamano hilo mjini Niamey.
Makubaliano hayo yanajiri baada ya miaka 17 ya mashauriano makali na yaliyoafikiwa rasmi mwishoni mwa mwezi Aprili wakati makubaliano hayo yalipovuka kiwango cha uzinduzi kilichohitaji kuratibishwa na angalau mataifa 22.
Nigeria, taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, ilitangaza wiki hii kwamba itajiunga na makubaliano hayo ya Niamey baada ya kujiondoa bila kutarajiwa mwaka jana.
from sokoa news https://ift.tt/2JhExAs
1


0 Comments