Wagonjwa wote wa UKIMWI kupatiwa tiba


Makamu wa rais wa Afrika Kusini Bw. David Mabuza ameahidi kuwa wagonjwa wote wa UKIMWI nchini humo watapata matibabu.

Bw. Mabuza ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa ripoti ya kimataifa ya mwaka 2019 ya UNAIDS uliofanyika Eshowe, jimbo la Kwazulu Natal nchini Afrika Kusini. Amesema hatua ya serikali ya kukabiliana na ugonjwa huo ni kuweka kipaumbele kazi ya kukinga na kuhakikisha wagonjwa wote wanapata matibabu.

Ripoti hiyo imeipongeza Afrika Kusini kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya UKIMWI na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa asilimia 40.

Afrika Kusini ni nchi yenye kiwango cha juu zaidi cha maambukizi ya UKIMWI duniani, ambapo hivi sasa nchini humo kuna zaidi ya watu milioni 4.2 wanapata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI.


from sokoa news https://ift.tt/2XPG4H0
1

Post a Comment

0 Comments