Waliofariki baada ya jengo kuwaka moto wafikia 33


Idadi ya vifo vilivyotokana na moto uliozuka katika studio Kyoto, Japan imeongezeka hadi kufikia 33 na wengine 36 kujeruhiwa, huku wengine kadhaa wakiwa katika hali mahututi.

Moto huo uliotokea katika jengo lenye ghorofa tatu ambao uliwashwa na mtu aliyekuwa kioevu kinachowaka moto.

Kwa mujibu wa Polisi mwanamume mwenye umri wa miaka 41, aliyetambuliwa na leseni yake ya udereva, alikubali kuwa alisababisha moto huo kwa kutumia kioevu kinachowaka moto, labda petroli, karibu na jengo hilo.




from sokoa news https://ift.tt/2JGPw6T
1

Post a Comment

0 Comments