Wananchi wa Kitongoji cha Kaugeri Kata ya Mwaru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wameshindwa kujizuia furaha yao na kujikuta wakimbeba na kusukuma gari la Mbunge wao Elibariki Kingu kutokana na jitihada zake za kuwapelekea miradi ya maendeleo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti jana kwenye mikutano ya hadhara aliyoandaa mbunge huyo katika vitongoji vya Kaugeri na Mlandala walisema haijawahi kutokea tangu vianzishwe vijiji hivyo kwa kupata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka minne tangu mbunge huyo aingie madarakani.
Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa wananchi wa kitongoji cha Kaugeri aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga alisema haijawahi tokea mbunge wa mfano kama Kingu.
”Mbunge huyu hana wa kumlinganisha naye amejitahidi sana kutuletea maendeleo katika Kata yetu yenye vitongoji vitano vya Kaugeri, Mdughuyu, Mlandala, Mpugizi na Mwaru."
Alisema katika vitongoji hivyo ameweza kujenga shule, zahanati na sasa amewaletea mradi mkubwa wa maji ambao utasambaza maji kwenye vitongoji vyote vya kata hiyo.
Diwani wa Kata hiyo Iddi Makangale alisema tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea Mbunge kama Kingu kwani kazi iliyofanywa na Rais John Magufuli na Mbunge huyo kwa kushirikiana na wananchi imewarahisishia upatikanaji wa kupata kura nyingi katika uchaguzi mkuu kwa chama chao cha Mapinduzi (CCM).
”Kwa kazi hii kubwa iliyofanyika hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi mnono ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya” alisema Makangale.
Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi hao na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha na kuzielekeza kwa wananchi wanyonge kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.
from sokoa news https://ift.tt/2M3Hg2q
1
0 Comments