KOCHA Mkuu wa timu ya Ruvu Shooting, Salum Mayanga, amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kuvaana na Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mayanga ambaye alichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Agosti, aliiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo amesema mbinu alizotumia katika mchezo huo, ndizo atazitumia tena kuibuka na ushindi dhidi ya Prisons.
Akizungumza na Champion Jumamosi, Mayanga alisema kuwa, jana Ijumaa walikuwa tayari wamefika jijini Mbeya kwa ajili mchezo huo.
“Kikosi kipo vizuri, tumeshafika Mbeya kuhakikisha tunapata pointi tatu kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga. Tulichokifanya siku ile ndicho tutakifanya safari hii.
“Nitamkosa kiungo wangu Zuberi Dabi ambaye ni majeruhi ingawa tayari ameshaanza mazoezi mepesi na amepangiwa programu maalumu kwa ajili ya kumsaidia aweze kurudi uwanjani haraka,” alisema Mayanga.
Abdulghafal Ally, TUDARCo
The post Mayanga Atumia Mbinu za Yanga Kuimaliza Prisons appeared first on Global Publishers.
from sokoa news https://ift.tt/32BWb8S
1
0 Comments