Ikufikie tu kuwa kocha mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi leo alfajiri amewasili nchini akitokea katika nchi ya Congo alikokuwa kwaajili ya majukumu ya timu ya Taifa.
Kocha huyo kuwasili kwake ni habari njema kwa wanaYanga kwani zilianza kuzuka taarifa kuwa anaweza asirejee tena nchini kuendelea kuifundisha Yanga.
Kocha huyo ataungana katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea kwaajili ya maandalizi ya mechi ya kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup mechi itakayofanyika 31 March 2019 katika uwanja wa CCM KIRUMBA.
0 Comments