WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe pamoja na Katibu wake, wametembelea viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya Afcon ya Vijana hapa nchini kuanzia Jumapili ya mwezi huu.
Viwanja ambavyo vimekaguliwa ni pamoja na Uwanja wa Taifa pamoja na Uwanja wa Azam ambavyo ni kwa ajili ya mechi huku ule wa Uhuru ukiwa ni kwa ajili ya mazoezi.
Mwakyembe amesema kuwa anaona ni hatua kubwa ambayo imefikiwa na Taifa pamoja na maandalizi kwenda sawa hali inayompa matumaini.
"Mabadiliko ambayo yanaonekana kwa sasa ni makubwa na ni hatua inayopaswa pongezi, nina imani vijana wetu watafanya kazi kubwa kupeperusha Bendera ya Taifa.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo Susan Mlawi amesema "Tulitenga jumla ya shilingi bilioni moja na milioni 300 kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vitakavyotumika na bilioni moja kwa ajili ya malazi, usafiri, chakula pamoja na vifaa vya ufundi ndani ya viwanja husika," amesema Mlawi.
0 Comments