Kenya kuchuana na Tanzania, Senegal na Algeria Afcon 2019

Timu ya taifa ya Kenya ina kibarua kigumu katika kombe la bara Afrika baada ya kupangwa kwenye kundi C pamoja na vigogo Senegal, Algeria na majirani Tanzania.

Senegal na Algeria wanapaniwa kufuzu kwenye robo fainali kutoka kundi C na hivyo Harambee Stars inafaa kujikakamua ili kuweza kupata nafasi katika robo fainali.

Majirani Uganda wana kibarua kigumu zaidi katika kundi A. Miamba hao wa Afrika Mashariki watachuana na wenyeji Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zimbawe.

Mabingwa watetezi Cameroon wako kwenye kundi F pamoja ma mibabe Ghana, Benin na Guinea Bissau.

Mabingwa wa 2013 Nigeria, wako kwenye kundi jepesi ambalo linajumuisha, Guinea, Madagascar na Burundi

Makundi yote

Kundi A: Egypt, DR Congo, Uganda, Zimbabwe

Kundi B: Nigeria, Guinea, Madagascar, Burundi

Kundi C: Senegal, Algeria, Kenya, Tanzania

Kundi D: Morocco, Ivory Coast, South Africa, Namibia

Kundi E: Tunisia, Mali, Mauritania, Angola

Kundi F: Cameroon, Ghana, Benin, Guinea Bissau




from sokoa news http://bit.ly/2v2CHM0
1

Post a Comment

0 Comments