Tanzania kupitia timu ya vijana ya Serengeti Boys inaenda kuweka historia kwa kuanza kufungua rasmi fainali za AFCON U-17 ambapo itamenyana na Nigeria majira ya saa kumi jioni huku mchezo wa usiku ukiwa Uganda dhidi ya Angola majira ya saa moja usiku yote Uwanja wa Taifa, Aprili 14.
Ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa mashindano makubwa ya namna hii ambayo yatatoa nafasi kwa timu kwenda Brazil katika kombe la Dunia endapo itashinda zaidi ya michezo miwili katika kundi sawa na alama 6.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harison Mwakyembe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ya Serengeti Boys.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yetu ya vijana, pia mashindano yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kujipanga,” amesema Mwakyembe.
Serengeti Boys wamekuwa katika wakati bora sana katika maandalizi yao, ambapo walienda kwenye mashindano maalum Uturuki, Rwanda na Kenya. Sehemu zote wamefanya vyema jambo linalotoa matumaini kwao na kwa Watanzania pia.
Viingilio vitakuwa Tsh 5,000 na 2,000.
from sokoa news http://bit.ly/2DeHYoi
1

0 Comments