Kikosi cha Simba kimewasili salama jijini Lubumbashi mashariki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuvaana na wenyeji wao TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi April 13 majira ya saa 10 jioni saa za Afrika Mashariki.
Simba wanaenda kucheza mchezo huo wakihitaji ushindi au sare yoyote ya magoli. Rekodi za Simba ugenini mwaka huu haziibebi sana licha ya kumbukumbu ya mwaka 2003 ya kuwatoa mabingwa wa Afrika Zamalek baada ya sare ya goli 1-1 kabla ya penalti kuamua.
Kuelekea mchezo huo kikosi cha Simba kilichotua Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni
1. Aishi Manula
2. Deogratius Munish
3. Juuko Murshid
4. Said Ndemla
5. Hassan Dilunga
6. Jonas Mkude
7. John Bocco
8. Clatous Chama
9. Erasto Nyoni
10. Paul Bukaba
11. James Kotei
12. Rashid Juma
13. Meddie Kagere
14. Emmanuel Okwi
15. Haruna Niyonzima
16. Mohammed Hussein
17. Zana Coulibaly
18. Mzamiru Yassin
from sokoa news http://bit.ly/2Gjopgz
1

0 Comments