Baada ya maumivu waliyopata katika mchuano wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wengi walitarajia kuona jinsi watakavyoshuka dimbani kwa mara nyingine na labda kulipiza kisasi.
Na baada ya kipyena cha mwisho kupulizwa, ilikuwa dhahiri kuwa angalau walijihisi wepesi moyoni na kutuliza maumivu hayo. Bao la kwanza la Phil Foden katika Ligi ya Premier liliwarejesha Manchester City kileleni mwa ligi baada ya kuwabwaga Tottenham Hotspur 1 – 0 uwanjani Etihad.
Bao la kichwa la Foden mwenye umri wa miaka 18, lililotengenezwa na Sergio Aguero, baada ya tu ya dakika tano lilihakikisha kuwa mabingwa hao watetezi waliendeleza shinikizo dhidi ya wapinzani Liverpool kabla ya kucheza mechi yao dhidi ya Cardiff City Jumapili.
from sokoa news http://bit.ly/2XrzXnB
1

0 Comments