Kagera Sugar yatakata mbele ya Simba katika ligi kuu

Klabu ya Simba imepoteza mchezo wa pili kwenye michezo 24 ya Ligi dhidi ya Kagera Sugar katika mtanange uliochezwa uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera ukiwa ni mchezo wa kiporo kwa timu ya Simba.

Kagera Sugar ikihitaji ushindi wowote ule kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara ililazimika kusubiri mpaka dakika ya 18 ya mchezo ambapo Kassim Hamis alikwamisha nyavuni mpira baada ya uzembe wa Paul Bukaba.

Katika dakika ya 41 ya mchezo Kagera Sugar walipata goli lingine kupitia kwa kinda wa timu hiyo Ramadhan Kapera ambaye ameibuka mchezaji bora wa mechi baada ya kufunga moja na kusaidia moja.

Mpaka kipyenga cha mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa dakika 45 za kwanza, Simba 2-0.

Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kadhaa ambayo yaliongeza nguvu kwa kikosi hicho kwa kumwingiza John Bocco, Hassan Dilunga yalisaidia kupatikana kwa goli kupitia kwa Emmanuel Okwi dakika ya 68. Mwamuzi Adongo anamaliza mpira Kagera Sugar 2 – 1 Simba.

Matokeo hayo yameifanya Kagera Sugar kupanda mpaka nafasi ya 13 kutoka 17 iliyokuwepo awali, wakati Simba ikisalia nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kipigo cha leo.

Kagera Sugar imekuwa na mwendelezo bora wanapocheza na Simba baada ya kuvunja mwiko wa kutopoteza kwa michezo tisa mfululizo, lakini pia msimu uliopita Simba ikiwa imetangazwa kama mabingwa wapya ilikutana na Kagera mbele ya mgeni rasmi Dkt Magufuli iliitungua Simba kwa goli moja kwa bila uwanja wa Taifa.




from sokoa news http://bit.ly/2Gy3NkJ
1

Post a Comment

0 Comments