Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana Serengeti Boys imehitimisha mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa kupoteza michezo mitatu yote.
Katika mchezo wa leo Jumamosi Serengeti Boys imekubali kipigo cha goli 4-2 dhidi ya Angola, mtanange uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ukiwa ni mchezo wa tatu baada ya ule wa Nigeria na Uganda, Tanzania imeshindwa kuambulia hata alama moja huku kila mmoja akisema lake.
Maoni: Sababu zilizopelekea kutofanya vizuri kwa Serengeti Boys:-
Mabadiliko ya kikosi. Kwa mwavuli wa kuimarisha kikosi, baadhi ya wachezaji waliokuwa na uelewano na wenzake kumepelekea timu hiyo kukosa kuelewana. Mfano Jefferson Olivestwist.
Ubora wa wapinzani. Nigeria ni mabingwa wa dunia kwa vijana, Uganda wameshatengeneza msingi bora wa vijana hali kadhalika kwa Angola ambao nao wameendelea sana kwa mpira wa vijana.
Shinikizo la kucheza nyumbani na ahadi zilizotolewa. Inawezekana isieleweke sana lakini vijana walicheza kwa hofu ya kutowaumiza Watanzania ikapotea, wengine zawadi ikipelekea kujipa nguvu pasipo.
Zipo sababu nyingi ambazo hazijabainishwa katika andiko hili lakini mwanga kwa Watanzania wasisite kuendelea kujiimarisha katika soka la vijana ambalo limekuwa nuru kwenye nchi zilizoendelea. Hii ni changamoto tu isiwakatishe tamaa.
from sokoa news http://bit.ly/2VVJvab
1

0 Comments