Safari ya Simba inafikia kikomo Lubumbashi

Safari ndefu iliyojaa vitimbi na mabonde mengi kwa klabu ya Simba imefikia tamati baada ya kukubali kipigo cha magoli 4-1 dhidi ya mabingwa mara tano wa Ligi ya mabingwa Afrika TP Mazembe kwenye mchezo uliopigwa Lubumbashi Congo.

Ikiwa katika jahazi, Simba ilifika eneo lisilo na hatua ya kurudi nyuma bali kusonga mbele tu, kutokana na mipango na mikakati ya timu hiyo. Mpango wa kwanza uliojazwa na hamasa umemezwa na kutokuamini katika kuweza, unaitwa “tulipanga kufika hatua ya makundi tumefika, huku ziada”.

Ndani ya mchezo kila timu ilipigwa na butwaa kutokana na goli la mapema la Emmanuel Okwi ambalo zote hazikuamini kilichotokea. Dakika ya pili tu Okwi aliitanguliza Simba kwa goli maridadi ingawa halikutosha kuipa ushindi.

Wakati kipindi cha kwanza kinaelekea mwishoni TP Mazembe ilipata goli la kwanza liloipa nguvu kupitia kwa Kabaso Chongo, baadae goli lingine Meshack Elia 38 akatia kimiani.

Kipindi cha pili kilimalizwa kupitia kwa goli la Tresor Mputu dakika ya 62 na Jackson Muleka dakika ya 74 ambayo yamefanya jumla ya goli 4-1 baada ya mtanange wa mkondo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam kuishia kwa sare ya  0-0.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuondoshwa kwenye michuano hiyo huku TP Mazembe ikifuzu hatua ya nusu fainali ambapo itacheza na mshindi kati ya CS Constantine au Esparance Des Tunis pamoja na zawadi ya fedha.

Aidha, mbali na kuondoshwa kwa Simba bado inatoa matumaini mema kwa siku sijazo kwani tangu ilipofanya vizuri mwaka 2003 ndio inafanya vizuri msimu huu, huku akizifunga timu kama Al Ahly, AS Vital na JS Soura.




from sokoa news http://bit.ly/2P83Eag
1

Post a Comment

0 Comments