AZAM FC: SMBA WANABAHATI LEO MVUA IMEWAOKOA, TULIDHAMIRIA KUWAUMBUA


KOCHA wa timu ya Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa leo Simba walikuwa wana bahati kwani walijipanga kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 mzunguko wa kwanza mvua imetibua mipango.

Azam FC leo wamegawana pointi moja na Simba uwanja wa Uhuru baada ya kushindwa kupata matokeo ndani ya dakika 90 baada ya kutoka na suluhu ya bila kufungana.

"Tulijipanga na tulidhamiria kushinda leo, hizo ndiyo zilikuwa hesabu zetu bahati mbaya mvua imetibua mipango yetu hali iliyofanya tugawane pointi moja.

"Tunaitambua Simba vizuri kutokana na uzoefu, kwa sasa tunaachana na mchezo wa leo hesabu zetu ni kulelekea michezo iliyobaki kwenye ligi," amesema Cheche.

Ushindi wa leo unaifanya Azam FC ijikite nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 36 ikiwa nafasi ya tatu imebakiwa na michezo miwili mkononi baada ya kucheza michezo 36 na ina pointi 69.



from sokoa news http://bit.ly/2JDj71a
1

Post a Comment

0 Comments