
Rome, Italia. Juventus imeanza vibaya matumizi ya jezi yake mpya, baada ya kufungwa na AS Roma katika mchezo wa Ligi Kuu Italia, juzi usiku.
Juventus ikiwa ugenini ilichapwa mabao 2-0 yaliyofungwa na nahodha Alessandro Florenzi dakika ya 11 kala ya nyota wa zamani wa Manchester City, Edin Dzeko kuongeza jingine dakika ya 87.
Pamoja na kipigo hicho, jezi ya timu hiyo iliteka mjadala nchini humo kutokana na aina ya rangi zake mbili tofauti nyeupe na nyeusi.
Kitendo cha kuwekwa rangi nyeupe upande wa kushoto na nyeusi kulia, kuliibua mjadala kuhusu utamaduni wa klabu hiyo kongwe Italia.
Pia matokeo hayo yamekuja wakati kukiwa na taarifa kocha wa timu hiyo, Massimiliano Allegri anajiandaa kuondoka Juventus.
Juventus ilianza mchezo kwa kasi na Cristiano Ronaldo alipiga kiki kali iliyotokana na mgongeo wa Juan Cuadrado lakini kipa Antonio Mirante aliokoaPia Ronaldo aliweka mpira kambani, lakini mwamuzi alikataa baada ya kujiridhisha kwa kutumia marudio ya picha kwa kutumia VAR.
Licha ya ushindi huo, AS Roma imebaki katika nafasi ya sita ikiwa na pointi sita katika msimamo wa Ligi Kuu. Juventus tayari wametwaa ubingwa.
from sokoa news http://bit.ly/2LFOH16
1

0 Comments