Sanchez aomba radhi Man United


London, England. Mshambuliaji nguli wa Manchester United, Alexis Sanchez ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kwa kushindwa kucheza kwa kiwango borab msimu huu.


Kauli ya Sanchez imekuja muda mfupi baada ya Man United kumaliza katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu England.


Majirani zao Manchester City walitwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya juzi kuichapa Brighton mabao 4-1.


Sanchez na wachezaji wenzake Man United wametupiwa lawama na mashabiki wa klabum hiyo kwa hatua yao ya kuboronga katika mashindano hayo msimu huu.


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, amekiri kupitia kipindi kigumu tangu alipojiunga na Man United akitokea Arsenal.


“Waandishi wa habari na watu wamekuwa wakizungumza tetesi, jambo ambalo si kweli. Naomba radhi mashabiki,”alisema Sanchez.


from sokoa news http://bit.ly/2WGQkwt
1

Post a Comment

0 Comments