Bilionea Maarufu hapa nchini Rostam Azizi imeelezwa kuwa amekusudia kuisaidia Yanga misaada ya kifedha pale inapowezekana. Hii inakuja siku chache tu baada ya Yanga kufanya uchaguzi na kupata viongozi wapya chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla na makamu wake Frederick Mwakalebela aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
0 Comments