Beki wa KMC Ally Ally ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakiwaniwa kusajiliwa na Yanga, hata hivyo mpango huo ulishindikana baada ya pande mbili kushindwa kufikia makubaliano
Licha ya uongozi wa Yanga kutoweka wazi michakato yake ya usajili, inafahamika Ally alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika mazungumzo na mabingwa hao wa kihistoria
Ally ametaja maslahi kuwa kikwazo kilichomkwamisha kutua Yanga
"Yanga walikuja na tulikaa nao mezani shida ni dau, mimi mpira ndio maisha yangu siwezi kucheza kwa maslahi madogo nina ndugu wananiangalia mimi, sina mkataba na timu nyingine yeyote naendelea na mazungumzo kuna baadhi ya timu zimenifuata," amesema
Hata hivyo inaelezwa Yanga iliachana na mpango wa kumsajili beki huyo baada ya kumnasa beki wa Kimataifa wa Burundi Mustapha Suleyman aliyetokea klabu ya Aigle Noir, mabingwa wa ligi kuu ya Burundi
Inaelezwa, Mustapha ambaye atashiriki michuano ya AFCON na kikosi cha Burundi, amesaini mkataba wa miaka miwili
from sokoa news http://bit.ly/2K6QzhK
1

0 Comments