Kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya Taifa ya Zimbabwe ambacho kitashiriki michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika nchini Misri
Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji watano waliojumuishwa kutoka kwenye kikosi kilichokuwa kinashiriki michuano ya COSAFA kuungaana na wengine 18 ambao walikuwa Nigeria kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria, mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Mlinda lango Elvis Chipezeze na mshambuliaji Nyasha Mushekwi anayecheza China ni mongoni mwa walioongezwa kwenye kikosi hicho
Kamusoko alionyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya COSAFA, kujumishwa kwake katika kikosi cha wachezaji 23 haishangazi
Kiungo huyo anayemaliza mkataba Yanga, bado haijafahamika kama atasalia Yanga au ataachwa
from sokoa news http://bit.ly/31nBPjS
1

0 Comments