Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amekiri kuwepo kwa mazungumzo ya mkataba mpya na nahodha wa timu hiyo Ibrahim Ajib

Hata hivyo amesema bado mchezaji huyo hajasaini

Jana zilisambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga, Makalebela amezikanusha taarifa hizo

"Bado tuko kwenye mazungumzo na Ajib, taarifa za yeye kusaini mkataba wa miaka miwili hazina ukweli wowote," amesema

Ajib akanusha kutua Simba

Wakati ikielezwa kuwa kiuungo huyo tayari amesaini mkataba wa awali kuitumikia Simba, Ajib amesema taarifa hizo hazina ukweli

"Sijasaini mkataba wa awali wala mkubwa na klabu ya Simba. Ukweli ni kwamba bado sijasaini Yanga wala Simba. Nasubiri kukamilika kwa mazungumzo yaliyopo, kila kitu kitakuwa hadharani baada ya muda mfupi. Naweza kucheza timu yoyote ikiwemo Yanga kama tutafikia makubaliano" amesema

Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kuhusu usajili wa kinara huyo wa kutoa pasi za mabao msimu uliomalizika

Awali aliondolewa kwenye mipango ya kocha Mwinyi Zahera baada ya kupata ofa ya kusajiliwa na TP Mazembe.

Hata hivyo baada ya dili hiyo kukwama, Yanga imeingia kwenye ushindani na wapinzani wao Simba kuwania saini yake kwa ajili ya msimu ujao


from sokoa news http://bit.ly/2I4zItC
1

Post a Comment

0 Comments