Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimewasili nchini Misri kuendelea na maandalizi ya michuano ya AFCON itakayoanza Juni 21 nchini humo
Ikiwa Misri, Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambapo Stars itashuka dimbani Juni 23 kuumana na Senegal
Nahodha wa Stars Mbwana Samatta amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri na anaamini watakuwa na maandalizi mazuri kabla ya kuanza michuano ya Afcon
Stars imetua Misri ikiwa na kikosi cha wachezaji 32. Kocha Emmanuel Amunike atachagua wachezaji 23 watakaoshiriki michuano hiyo
from sokoa news http://bit.ly/2WY3JUc
1

0 Comments