"Vijana ndiyo mkono wa kiume katika chama " Joan Faith Kataraiya




Na Clavery Christian Bukoba.

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa umoja wa vijana UVCCM taifa bi, Joan Faith Kataraiya amemkabidhi bendera 400 mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM taifa bw,  Khery James ili ziweze kugawiwa katika wajumbe wa mashina ambao wanaitwa mabarozi kwa ajiri ya kuongeza amsha amsha katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi wa kumi mwaka 2019.

Bi, Johan Kataraiya amewataka viongozi wenzake ndani ya chama kuhakikisha wanakipigania chama kila mmoja kwa nafasi yake ambapo amesema kuwa vijana katika chama ni kama mkono wa kuume kwa mwanadamu.

Aidha amesema kuwa ameamua kutoa bendera hizo yeye kama mwakilishi wa vijana katika kuongeza hamasa kwa vijana wenzake kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hasa nafasi za uenyeviti wa serikali za mitaa na nyinginezo.

Bi Johan amekabidhi bendera hizo katika uzinduzi wa Kagera ya kijani ambayo imezinduliwa rasmi mkoani Kagera na M/kiti wa umoja wa vijana uvccm taifa bw, Kheri James katika uwanja wa hamgembe bukoba ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa.


from sokoa news https://ift.tt/32ZR8QT
1

Post a Comment

0 Comments