Wananchi Liwale watoa ekari 50 kupisha ujenzi wa hospitali



Na Ahmad Mmow, Lindi.

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, wananchi wa wilaya ya Liwale wametoa ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.

Hayo yalielezwa jana na mkuu wa wilaya hiyo, Sarah Chiwamba alipozungumza na Muungwana Blog, mjini Liwale.

Chiwamba ambae wilaya yake imefanikiwa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito kutoka vifo nane mwaka 2017/2018 hadi vitatu mwaka 2018/2019, alisema tatizo la ufinyu wa eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya limepata suluhisho.

Baada ya wananchi kukubali kuachia maeneo bila malipo (fidia) ili kupisha ujenzi huo. 4: Alisema wananchi hao kwakutambua umuhimu wa hospitali hiyo ambayo ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni,  wamekubali kutoa maeneo yao yenye jumla ya ekari 50 katika kata ya Liwale B.

''Ujenzi utaanza mapema baada ya kumaliza hatua za usafi wa eneo, na hivi tunavyowasiliana nawe usafi unaendelea. Tumepata eneo la ekari hamsini katika kata ya Liwale B ambayo haiko mbali na makao makuu ya wilaya. Eneo limeshapimwa na mipaka inajulikana na hakuna masuala ya fidia, kwani wananchi wamekubali kutoa eneo hilo bure ili wajengewe hospitali mpya ya wilaya,'' alisema Chiwamba.

Mkuu huyo wa wilaya ya Liwale iliyopo mkoani Lindi, alisema hatua hiyo imetokana na hospitali ya wilaya hiyo ambayo awali ilikuwa kituo cha afya kuwa na eneo dogo.

Huku akiweka wazi kwamba katika mwaka huu wa fedha (2019/2020) serikali  imetenga shilingi milioni 500 zitakazo tumika kwa ujenzi huo.

Kuhusu sababu  zilizochangia wilaya hiyo kufanikiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kuwa ni wilaya kuongezewa  watumishi wenye weledi katika vituo vya kutolea huduma za afya, kuongezwa kwa watumishi 83 wa kada mbalimbali katika sekta ya afya, elimu kwa jamii na kutoa huduma mkoba kwa maeneo yaliyo mbali na vituo vya kutolea huduma.

Sio hayo tu yaliyochangia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito. Lakini pia  mfumo mzuri wa rufaa kwa wagonjwa kutoka kwenye vituo ya kutolea huduma kuja wilayani kwa kuhakikisha mafuta yanapatikana wakati wote na  matengenezo ya haraka ya magari  ya kubebea wagonjwa ni sehemu ya mchango wa mafanikio hayo,'' Chiwamba alifichua baadhi ya siri za mafanikio hayo.

Wilaya ya Liwale ambayo vituo vyake vya afya vya Mpengere na Kibutuka vinatarajiwa kuanza kutoa huduma mwezi Agosti, mwaka huu, inavituo 37 vya kutolea huduma za afya.


from sokoa news https://ift.tt/336tke6
1

Post a Comment

0 Comments