TAARIFA ikufikie kwamba kila ukimuona Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera akitinga uwanjani basi tambua kuwa zaidi ya Sh Mil 1 imekatika kwa mavazi tu.
Zahera ambaye amejizolea umaarufu kutokana na mavazi yake ya kipensi, amesema kwamba licha ya watu kuona anavaa vitu vichache lakini vina gharama kubwa sana kuvinunua.
Pamoja na hilo, hivi karibuni Zahera mwenye uraia wa Ufaransa alijikuta akitozwa faini ya Sh 500,000 kutokana na kuvaa mavazi yanayotajwa kuwa siyo nadhifu kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa ni kinyume cha kanuni 14 (2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu ilitolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41 (13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha. Championi Jumamosi lilikutana uso kwa uso na Zahera ambaye aliweka wazi kuwa pamoja na watu kumchukulia poa kwa mavazi yake lakini amekuwa akitoa fedha nyingi sana kuyanunua. Zahera alifafanua gharama za mavazi yake:
“Hii kofi a tu kuipata ni euro 120 (Tsh 303,331), nguo ya chini (kipensi) euro 90 (Tsh 227,498) na fulana ni euro 400 (Tsh 1,011,100). Fedha ambazo ukizijumlisha zote unapata kitita cha Tsh 1,541,929.
“Mnazidharau lakini hizi ni nguo za hela nyingi sana,” alisema Zahera.
MWANDISHI WETU, Dar es Salaam
The post Kipensi Zahera Akitinga Taifa… Milioni Imeteketea appeared first on Global Publishers.
from sokoa news https://ift.tt/34HBfzc
1
0 Comments