
MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shaaban Chilunda, amesema hana mpango wa kucheza katika klabu yoyote hapa nchini kwani malengo yake ni kuendelea kucheza soka la kulipwa nje.
Chilunda alikuwa akicheza katika klabu ya Tenerife ya Hispania, lakini baadaye walimtoa kwa mkopo kwenye klabu ya Ligi Daraja la Kwanza ya CD Izarra pia ya nchini humo, ila kwa sasa amevunja mkataba.
Awali, Chilunda alikuwa ni mchezaji wa Azam FC ambao walimuuza katika klabu hiyo ya Tenerefe.
Akizungumza nasi jijini Dar es Salaam jana, Chilunda alisema kwa sasa nguvu zake anazielekeza katika timu ya Taifa inayokabiliwa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon2019), nchini Misri.
“Licha ya kuvunja mkataba na klabu ya Tenerife, sina mpango wowote wa kuendelea kucheza hapa Tanzania kwani naangalia nipate timu nyingine nje ya nchi,” alisema.
Alisema anahitaji kucheza soka la kulipwa ili aweze kutangaza vema jina lake japo hakuweza kupata nafasi ya kucheza katika klabu yake ya Tenerife.
Kuna habari kuwa klabu kongwe hapa nchini, Simba na Yanga na Azam FC, zimeanza kumwinda mchezaji huyo, kuelekea usajili wa msimu ujao.
from sokoa news http://bit.ly/2EYqYmV
1

0 Comments