Ngasa asubiri mkataba mpya Yanga



Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema bado anasubiri ofa kutoka kwa vigogo kabla ya kufanya uamuzi ya kutimkia kwingine.

Ngassa alisema kipaumbele atatoa kwanza kwa Yanga kama hawataonyesha uhitaji wa kutaka kuendelea naye atatimkia kwingine kukabiliana na changamoto mpya za soka.

"Nina ofa zaidi ya mbili lakini siwezi kufanya uamuzi ya kuondoka ghafla nitakuwa sio muungwana kwa waajiri wangu ambao mkataba nao umemalizika"

"Siku zio nyingi nitakaa nao ili kujua mustakabali wangu mapema, kuhusu mahusiano yangu na kocha ni mazuri na kwa kipindi chote ambacho nimecheza chini yake tumekuwa tukifanya kazi vizuri," Ngasa aliliambia Mwanaspoti

Akiizungumzia nafasi ambayo Yanga wameipata msimu ujao ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, winga huyo alisema ni nafasi ambayo kila mchezaji ameifurahia.

"Niliipokea kwa furaha taarifa ya kurejea kwetu katika mashindano ya kimataifa, kama nitaendelea kuwa Yanga ni wakati wa kushirikiana na wachezaji wenzangu ili tuitetea nembo ya klabu yetu" alisema Ngassa.

Ngasa ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga msimu uliomalizika, akiisaidia timu kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimammo wa ligi pamoja na kufika nusu fainali michuano ya kombe la FA


from sokoa news http://bit.ly/2F0LEuq
1

Post a Comment

0 Comments