Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera ametoa agizo la kurudishwa kwa mtumishi mmoja aliyekuwa Afisa Ardhi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda bwana Peter Mkalipa baada ya kuisababishiaa hasara ya shilingi Milioni 36.
Kwa sasa Mtumishi huyo amehamishiwa wilaya ya Sengerema ambapo inadaiwa kuwa akiwa Mpanda aligawa viwanja vya Halmashauri vilivyopimwa ambapo kiwanja kimoja aligawa kwa zaidi ya mtu mmoja hali iliyosababisha migogoro ya ardhi.
Homera ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa katika baraza la hoja la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda.
Amesema mtumishi huyo alifanya hivyo kwa makusudi hivyo anawajibika kuja kujibu hoja hivyo amelitaka baraza la madiwani kumuandikia barua ya kumuita
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa wa Manispaa ya Mpanda bwana William Mbogo amekiri kuwepo kwa migogoro ya ardhi kutokana na watu kugonganishwa katika kiwanja kimoja
Hata hivyo ametoa tahadhari kwa watumishi kutokuzoea tabia hiyo ambayo ameiita ya makusudi na inaweza kuepukika
Bwana Michael Nzyungu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amesema Manispaa hiyo ilikuwa inakabiliwa na matatizo makubwa ya migogoro ya ardhi lakini kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wanaendelea kuyatatua.
Ameongeza kuwa ratiba za Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na Mkuu wa mkoa wa Katavi za kusikiliza kero za wananchi zinasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero za wananchi.
Awali katika kikao hicho Mkaguzi wa nje wa hesabu za serikali bwana Mohamed Msangi amesema kwa mwaka 2017/2018 halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imepata hati safi.
Bwana msangi ameongeza kuwa kati ya hoja 125 zilizowasilishwa; hoja 76 zina majibu ya kuridhisha na zimefungwa na hoja 49 zimeendelea kusalia.
from sokoa news https://ift.tt/2OqjGzD
1
0 Comments