Washiriki tamasha la kuendesha baiskeli wakiwa uchi


Watu washiriki tamasha la kuendesha baiskeli wakiwa uchi kwenye barabara za mji wa Vancouver, nchini Canada. Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka kama kampeni dhidi ya uchafuzi wa hewa na kuleta uhamasishaji wa mazingira.

Wanaoshiriki tamasha hilo wanahitajika kuenda uchi bila nguo yoyote au kupamba mwili wao na maandishi au rangi ya kuvutia.

Aidha waandalizi wa tamasha hilo huhimiza wanaoshiriki kusalia na nguo zao hadi tamasha linapoanza na pia kuzivaa mara moja tamasha linapokamilika ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.




from sokoa news https://ift.tt/330mJSk
1

Post a Comment

0 Comments