Wagiriki wanapiga kura leo katika uchaguzi, ambao uchunguzi wa maoni unaonesha unaweza kuwaingiza madarakani wapinzani wa kihafidhina na kuufikisha kikomo utawala wa miaka minne wa siasa za mrengo wa shoto ambao unalaumiwa kwa kuliingiza taifa hilo katika madeni zaidi na migogoro ya usimamizi mbaya.
Kwa kiasi kikubwa uchaguzi huo ni wa kujipima mabavu kwa wagombea wawili. Waziri Mkuu aliye madarakani Alexis Tsipras, mwenye umri wa miaka 44 akipeperusha bendera ya chama cha Syriza, ambae amekuwa madarakani tangu mwaka 2015 na kwa upande mwingine Kyriakos Mitsotakis, mwenye umri wa miaka 51, yeye wa chama cha New Democracy.
Mgombea huyo anatoka katika familia yenye mizizi ya kisiasa na ana matumani ya kufuata nyayo za baba yake aliyewahi kuwa waziri mkuu na dada yake waziri wa mambo ya nje. Uchunguzi wa maoni unatoa nafasi kwa chama cha New Democracy, kikiongoza kwa asilimia 10, ambazo kimsingi zinatoa ushindi mkubwa wa viti 300 vya ubunge.
Zoezi la upigaji kura linatarajiwa kuanza saa moja Asubuhi na kumalizika saa moja usiku, ambapo matokeo yake yanatarajiwa kuanza kutangazwa masaa mawili baada ya zoezi hilo kumalizika.
from sokoa news https://ift.tt/2YDidGJ
1


0 Comments